Seifeddine Rezgui, mshambuliaji wa Tunisia aliyewaua watu 38 katika
mgahawa wa kifahari eneo la Sousse anaaminika kupata mafunzo ya vita
nchini Libya.
Wizara ya ndani imesema kwamba Rezgui amekuwa nchini Libya tangu mwezi
Januari sawa na wanaume wawili walioshambulia makavazi mjini Tripoli
mwezi Machi. Wengi waliouawa kwenye shambulio la Sousse ni watalii
wakiwemo Waingereza 30.
Kundi la Islamic State limekiri kuhusika na shambulio hilo.Rezgui
alipata mafunzo ya itikadi kali wakati akisomea shahada ya uhandisi.
Tayari
maafisa wa Tunisia wamewakamata washukiwa kadhaa wanaodaiwa
kushirikiana na mshambuliaji huyo. Rais wa Tunisia Beji Caid Essebsi
amekiri kwamba maafisa wa usalama hawakutarajia shambulio kama hilo.
No comments:
Post a Comment