Mawaziri wa fedha kutoka kanda inayotumia sarafu ya Euro wanakutana
kutathmini ombi la Ugiriki kupewa mkopo wa dharura baada ya mamlaka za
Athens kushindwa kulipa deni lake kwa Shirika la Fedha DunianiIMF.
Hapo Jumanne Mawaziri hao walikataa kutoa fedha za kuukwamua uchumi wa Ugiriki baada ya mazungumzo kuvunjika.
Ugiriki
imekuwa nchi ya kwanza katika Muungano wa Ulaya kushindwa kulipa deni
lake kwa IMF. Msukosuko wa sasa wa kifedha imezua hofu huenda Athens
ikalazimika kujiondoa kutoka kanda inayotumia sarafu ya Euro.
Mkutano wa Jumatano utaamua ikiwa Ugiriki itapokea mkopo wa
dharura. Aidha Ugiriki pia imeomba kupewa fedha zaidi kuuchepua uchumi
wake.
Katika kipindi cha miaka miwili Ugiriki imepokea Euro
bilioni 29.1.
No comments:
Post a Comment