Idara ya umoja mataifa ya kuhudumia watoto UNICEF, inaonya kwamba
mamillioni ya watoto katika taifa lililokumbwa na vita la Yemen
wanatishiwa na utapia mlo na wako katika hatari ya kukumbwa na
magonjwa mabaya yanayoweza kuzuilika kama vile surua ya homa ya mapafu.
Vita nchini Yemen vinasababisha athari mbaya kwa watoto nchini humo.
Ripoti ya UNICEF inaeleza kuwa, takriban watoto 279 wameuwawa na wengine
402 kujeruhiwa tangu mwishoni mwa mwezi marchi, pale Saudia Arabia
ilipoanza kampeni yake ya mashambulizi ya anga dhdi ya waasi wa
Kihouthi.
Imeripotiwa kuwa watoto takriban 318 wameandikishwa kama
wanajeshi, lakini inasema inaamnini idadi ya kweli ya waioandikishwa ni
kubwa Zaidi.Wakati takwimu hizo zinashutusha, UNICEF inasema watoto pia
wanakabiliwa na hatari za magonjwa na utapia mlo. Msemaji wa UNICEF
Christof Boulierac, anasema watoto wako hatarini kupata magonjwa
yanayoweza kuzuilika kwa sababu hawajapatiwa chanjo.Kwasababu ya mzozo, Boulierac anasema vituo vya afya havina umeme
wala mafuta wanayohitaji kuhifadhi chanjo kwenye mahala baridi. Anasema
watoto wengi pia wanakosa chanjo za kuokowa maisha kwa sababu wazazi wao
mara nyingi wanakhofia mapigano kuwapeleka kupata chanjo.UNICEF inasema idadi ya watoto waliokumbwa na maambukizo ya mabaya ya
magonjwa hatari ya kupumua imeongezeka maradufu hadi watoto millioni
1.3 tangu marchi. Hii inaashiria ongezeko kubwa lakutokuwa na uwezo kwa
watoto kupata matibabu yanayohitajika kwasababu mahospitali na kliniki
hazifanyi kazi sawa sawa.Ripoti inasema maji machafu , hali duni za usafi wa vyoo na ukosefu wa
madini ya chumvi mwilini kunawaweka watoto zaidi ya millioni 2.5
katika hatari ya kupata magonjwa ya kuharisha, ambayo mara nyingi ni
hatari. Boulierac anasema utapia mlo pia ni tishio linaloongezeka.
No comments:
Post a Comment