Makundi ya wapiganaji yamefanya misururu ya mashambulio dhidi ya maafisa wa usalama nchini Misri katika Rasi ya Sinai.
Jeshi limesema makabiliano yanaendelea huku wanajeshi kadhaa na
wapiganaji wakiuawa.Taarifa ya jeshi imesema vizuizi vitano vya polisi
vililengwa sawa na kituo kimoja cha polisi.
Hili ndilo shambulio kubwa zaidi kufanywa na wapiganaji wa kiisilamu
walioko eneo la Sinai, miaka miwili baada ya kuondolewa madarakani kwa
Rais aliyeegemea mrengo wa kidini Mohamed Morsi.
Tukio hili
limejiri siku moja baada ya Rais wa Misri Abdul Fattah al Sisi kuapa
kupendekeza sheria mpya za kukabiliana na ugaidi. Hapo Jumatatu
mwendesha mashtaka wa Misri aliuawa katika shambulio la bomu iliyotegwa
ndani ya gari.
No comments:
Post a Comment