Marekani na Cuba zinatarajiwa kutangaza kufunguliwa kwa afisi za ubalozi
katika miji mikuu pande zote ikiwa ni hatua kubwa ya kurejesha uhusiano
wa kidiplomasia kati ya nchi mbili.
Uhusiano kati ya Marekani na Cuba ulivunjika miaka ya sitini na Marekani
iliiwekea Cuba vikwazo vya silaha. Hata hivyo nchi hizo zilikubaliana
kurejesha uhsuano mwishoni mwa mwaka 2014.
mwezi Aprili Rais Barack Obama wa Marekani na mwenzake wa Cuba Raul
Castro walifanya mazungumzo ya ana kwa ana ikiwa ni mara ya kwanza kwa
nusu karne.
Marekani ilivunja uhusiano wake na Cuba mwaka 1959
baada ya Fidel Castro na Kakake Raul Castro kuongoza mapinduzi
ualiyomuondoa madarakani Rais aliyeungwa mkono na Marekani Fulgencio
Batista.
No comments:
Post a Comment