Wanajeshi wa umoja wa Afrika nchini
Somalia Amisom hawataondoka katika miji yoyote ya kusini mwa Somalia
kinyume na ripoti za vyombo vya habari,kwa mujibu wa Amisom
Kumekuwa
na ripoti kwamba wanajeshi hao wamekuwa wakiondoka katika miji mitano
ya Somalia,lakini mwakilishi wa Umoja huo nchini Somalia balozi Maman
Sidikou amesema kuwa huo ni uvumi unaolenga kuzua hofu.Ameongezea kuwa vikosi vya AU vinapangwa kuendeleza vita dhidi ya kundi la La Alshabaab.
"wanajeshi wa umoja wa Africa wasita kuondoka Somalia"