Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limewawekea vikwazo ikiwemo
marufuku ya usafiri na kupiga tanji mali za majenerali sita wa Sudan
Kusini.
Watatu ni kutoka upande wa serikali na wengine watatu ni kutoka upande wa waasi.
Hatua hii inajiri siku chache baada ya ripoti mpya ya Umoja wa
Mataifa kuonyesha ukatili mkubwa wa kibinadamu katika mapigano
yanayoendelea nchini humo.
Mjumbe wa Marekani katika Umoja wa
Mataifa Samantha Power amesema vikwazo hivyo ni onyo kwa wale
wanaendeleza ukiukaji wa kibinadamu Sudan Kusini.
"VIKWAZO KWA MAKAMANDA WA SOUTH SUDAN"