Wednesday, July 1, 2015

"Mazungumzo zaidi ya kuinusuru Ugiriki"

Mawaziri wa fedha kutoka kanda inayotumia sarafu ya Euro wanakutana kutathmini ombi la Ugiriki kupewa mkopo wa dharura baada ya mamlaka za Athens kushindwa kulipa deni lake kwa Shirika la Fedha DunianiIMF.

Hapo Jumanne Mawaziri hao walikataa kutoa fedha za kuukwamua uchumi wa Ugiriki baada ya mazungumzo kuvunjika.
Ugiriki imekuwa nchi ya kwanza katika Muungano wa Ulaya kushindwa kulipa deni lake kwa IMF. Msukosuko wa sasa wa kifedha imezua hofu huenda Athens ikalazimika kujiondoa kutoka kanda inayotumia sarafu ya Euro.
Mkutano wa Jumatano utaamua ikiwa Ugiriki itapokea mkopo wa dharura. Aidha Ugiriki pia imeomba kupewa fedha zaidi kuuchepua uchumi wake.
Katika kipindi cha miaka miwili Ugiriki imepokea Euro bilioni 29.1.

0 comments:

Post a Comment