Wednesday, July 1, 2015

"Mamillioni ya watoto Yemen watishiwa na magonjwa"

Idara ya umoja mataifa ya kuhudumia watoto  UNICEF, inaonya kwamba mamillioni ya watoto katika taifa lililokumbwa na vita la Yemen wanatishiwa na utapia mlo na wako  katika hatari ya kukumbwa na  magonjwa mabaya yanayoweza kuzuilika kama vile surua ya homa ya mapafu.
 Vita nchini Yemen vinasababisha athari mbaya kwa watoto nchini humo. Ripoti ya UNICEF inaeleza kuwa, takriban watoto 279 wameuwawa na wengine 402 kujeruhiwa tangu mwishoni mwa mwezi marchi, pale Saudia Arabia ilipoanza kampeni yake ya mashambulizi ya anga dhdi ya waasi wa Kihouthi.
Imeripotiwa kuwa watoto takriban 318 wameandikishwa kama wanajeshi, lakini  inasema inaamnini idadi ya kweli ya waioandikishwa ni kubwa Zaidi.Wakati takwimu hizo zinashutusha, UNICEF inasema watoto  pia wanakabiliwa na hatari za magonjwa na utapia mlo. Msemaji wa UNICEF Christof Boulierac, anasema watoto wako hatarini kupata magonjwa yanayoweza kuzuilika  kwa sababu hawajapatiwa  chanjo.Kwasababu  ya mzozo, Boulierac anasema vituo vya afya havina umeme wala mafuta wanayohitaji kuhifadhi chanjo kwenye mahala baridi. Anasema watoto wengi pia wanakosa chanjo za kuokowa maisha kwa sababu wazazi wao mara nyingi wanakhofia mapigano kuwapeleka kupata chanjo.UNICEF inasema idadi ya watoto waliokumbwa na maambukizo ya mabaya ya magonjwa hatari ya kupumua imeongezeka maradufu hadi watoto millioni 1.3 tangu marchi. Hii inaashiria ongezeko kubwa lakutokuwa na uwezo kwa watoto kupata matibabu yanayohitajika kwasababu mahospitali na kliniki hazifanyi kazi sawa sawa.Ripoti inasema maji machafu , hali duni za usafi  wa vyoo na ukosefu wa madini ya chumvi mwilini  kunawaweka  watoto  zaidi ya millioni 2.5  katika hatari ya kupata magonjwa ya kuharisha, ambayo mara nyingi  ni  hatari. Boulierac anasema utapia mlo pia ni tishio linaloongezeka.

0 comments:

Post a Comment