BARAZA Kuu la Waislamu Tanzania (Bakwata) limemtangaza Shehe Abubakar
Zuberi Ally kuwa Kaimu Shehe Mkuu na Mufti wa Tanzania kufuatia kifo
cha aliyekuwa Mufti Shehe Shaaban Issa bin Simba kufariki dunia wiki
moja iliyopita.
Shehe Zuberi, atashika wadhifa huo kwa siku 90 ili kupisha uchaguzi
utakaofanyika kumpata kiongozi huyo mkuu wa Waislamu nchini kwa mujibu
wa taratibu za Kiislamu.
Uteuzi huo ulifanyika na kutangazwa jana asubuhi Bagamoyo, Pwani mara
baada ya Baraza la Ulamaa lenye wajumbe 7 kukaa na kumteua Shehe Zuberi
kushika wadhifa huo.
No comments:
Post a Comment