KAMANDA wa Polisi mkoani Arusha, Liberatus Sabas, amesema kuwa tuhuma
alizotoa Mbunge wa Arusha mjini, Godbless Lema si za kweli.
Kamanda huyo alisema madai kwamba polisi wanamuonea Lema kwa
kumkamata na kumweka mahabusu wakati yeye siyo mhalifu siyo za kweli na
kwamba yeye (Lema) ni chanzo cha vurugu katika uandikishwaji wa daftari
la wapigakura.
Akizungumza jana kwa njia ya simu jana Sabas alisema Lema
anasababisha vurugu kwa kutembelea maeneo ambayo watu wamejitokeza na
kujiandikisha na kuanza kupiga hotuba kitu ambacho kinyume cha sheria.
Alisema Lema kama anataka kuhamasisha watu hatukatai, aende maeneo
ambayo daftari bado halijafika akahamasishe na likifika aache wananchi
wajiandikishe na siyo kuwafuata kwenye mistari na kuanza kupiga hatuba,
siyo sahihi.
Alisema polisi hawawezi kuonea mtu wala yeye mbunge, isipokuwa
likipata taarifa kama siku ya tukio ya Juni 20 alipokamatwa kuwa analeta
vurugu na wananchi hawataki kumwona katika maeneo ya uandikishaji ndipo
walipokwenda kumkamata.
Alisema siku ya tukio walipata taarifa toka kwa askari walioko doria
kwenye kituo cha Osunyai kuwa kuna vurugu toka kwa mbunge na kuomba
ulinzi uongezwe na askari wakapelekwa zaidi na kumtia mbaroni na wenzake
24 na kuwa jumla ya watuhumiwa 25 walikamatwa na siyo yeye aliyetoa
taarifa Polisi kuomba ulinzi.
No comments:
Post a Comment