KAMANDA wa Polisi mkoani Arusha, Liberatus Sabas, amesema kuwa tuhuma
alizotoa Mbunge wa Arusha mjini, Godbless Lema si za kweli.
Kamanda huyo alisema madai kwamba polisi wanamuonea Lema kwa kumkamata na kumweka mahabusu wakati yeye siyo mhalifu siyo za kweli na kwamba yeye (Lema) ni chanzo cha vurugu katika uandikishwaji wa daftari la wapigakura.
Akizungumza jana kwa njia ya simu jana Sabas alisema Lema anasababisha vurugu kwa kutembelea maeneo ambayo watu wamejitokeza na kujiandikisha na kuanza kupiga hotuba kitu ambacho kinyume cha sheria.
Alisema Lema kama anataka kuhamasisha watu hatukatai, aende maeneo ambayo daftari bado halijafika akahamasishe na likifika aache wananchi wajiandikishe na siyo kuwafuata kwenye mistari na kuanza kupiga hatuba, siyo sahihi.
Alisema polisi hawawezi kuonea mtu wala yeye mbunge, isipokuwa likipata taarifa kama siku ya tukio ya Juni 20 alipokamatwa kuwa analeta vurugu na wananchi hawataki kumwona katika maeneo ya uandikishaji ndipo walipokwenda kumkamata.
Alisema siku ya tukio walipata taarifa toka kwa askari walioko doria kwenye kituo cha Osunyai kuwa kuna vurugu toka kwa mbunge na kuomba ulinzi uongezwe na askari wakapelekwa zaidi na kumtia mbaroni na wenzake 24 na kuwa jumla ya watuhumiwa 25 walikamatwa na siyo yeye aliyetoa taarifa Polisi kuomba ulinzi.

POLISI WAKANUSHA KUMUONEA LEMA