Monday, June 22, 2015

MITANDAO YA IS KUKABILIWA ULAYA

Kitengo cha polisi wa Ulaya kinabuniwa ili kuwatambua watu wanaotumia mitandao ya kijamii kuwaingiza vijana wa kiislamu kupigania Islamic State.
 Kitengo cha Ulaya cha polisi Europol kinasema kuwa kuna zaidi ya ujumbe laki moja katika twitter unaotumwa kila siku katika kurasa zinazohusiana na kundi hilo ambalo linathibiti Syria na Iraq.
Kitengo hicho kipya kitajaribu kufutilia mbali kurasa za IS kwa muda wa saa mbili pindi zinapotambuliwa.
Europol inaamini kuwa zaidi ya raia elfu tano wa muungano wa ulaya kutoka nchi za Uingereza, Ufaransa, Ubelgiji na Uholanzi wamezuru maeneo yanayotawaliwa na Islamic State.

0 comments:

Post a Comment