Watu wawili Maxmillian Rafael Msacky na Mfanyakazi wa Raha Patrick
James Natala, leo wamefikishwa katika Mahakama ya Kisutu wakishitakiwa
kwa makosa ya kughushi na kuunda mtandao feki kwa kutumia majina ya
Taasisi, Viongozi na Wanasiasa.
Mbele ya Hakimu Mkazi Emillius Mchauru, Mwendesha Mashitaka Theophil Mutakyawa amesema washitakiwa walitenda makosa hayo kwa nyakati tofauti kati ya Januari na April 2014 jijini Dar es Salaam, kinyume na Sheria ya Kielekroniki na Mawasiliano ya Posta namba 3 ya 2010.
Upande wa mashitaka umedai kuwa washitakiwa walitengeneza tovuti feki wakitumia majina ya Hisa Tanzania, Jakaya Foundation, Ridhiwani Social Company, TCRA Foundation.
Washitakiwa wote wamekana mashitaka na wamerejeshwa rumande baada ya kushindwa kutimiza masharti ya dhamana.
Upande wa mashitaka umesema uchunguzi bado haujakamilika na washitakiwa watafikishwa mahakamani tarehe 28 Septemba kesi yao itakapotajwa tena.

"Kizimbani kwa kughushi wavuti feki na kutumia majina ya Taasisi na wanasiasa"