Wednesday, August 5, 2015

"BOTI ILIYOJAA WAHAMIAJI KUZAMA LIBYA"

Waokoaji wanaendelea na shughuli ya kuwasaka mamia ya wahamiaji waliotumbukia baharini baada ya boti walimokuwa wakisafiria kwenda Ulaya kuzama majini katika bahari ya Mediterrania karibu na ufuo wa Libya.
Ripoti zinasema kuwa takriban watu 700 walikuwa kwenye mtumbwi huo uliozama baada ya kukumbana na mawimbi makali.
Wanajeshi wa majini kutoka Ireland wanakisia kuwa idadi kubwa ya watu wamekufa maji.
Aidha shirika la madaktari wasiokuwa na mipaka Medecins Sans Frontieres (MSF) limeonya kuwa huenda kukazuka maafa makubwa kufuatia idadi kubwa ya abiria waliokuwa kwenye mtumbwi huo uliozama.
Inakisiwa kuwa takriban wahamiaji 2,000 walikufa maji kwanza mwanza wa mwaka huu wakijaribu kufika ulaya kupitia bahari hiyo ya Mediterranea
Meli nne za uokozi na ndege tatu zimetumwa huko kujaribu kunusuru maisha ya wahamiaji hao.

0 comments:

Post a Comment