Tuesday, July 14, 2015

"Mtoto aliyekosha ulimwengu apewa msaada"

www.pewainformation.blogspot.com
Mtoto wa miaka 9 aliyepigwa picha nje ya mgahawa wa Mac Donalds huko Ufilipino anaendelea kupokea msaada utakaomsaidia atimize ndoto yake ya kupata elimu.

Daniel Cabrera alipigwa picha akiwa nje ya duka maarufu la Mac Donalds amejikunyata kwenye kibao anachokitumia kama meza ya kuwekea vitabu vyake akifanya mabaki ya kazi aliyopewa shuleni.
Cabrera alikuwa akitumia mwangaza wa bango la kutangaza duka la McDonald kama taa yake akidurusu !
Mwanafunzi wa Uuguzi bi Joyce Torrefranca, ndiye aliyeipiga picha hiyo nje ya mkahawa huo McDonald ulioko katika mji wa Cebu nchini Ufilipino na akaichapisha kwenye mtandao wake wa kijamii wa Facebook na ujumbe
''mtoto huyo amenikumbusha niwekee bidii maishani''
''kwangu mimi kama mwanafunzi ,nilipigwa na mshangao kutokana na ari ya mwanafunzi huyu mdogo aliyekuwa amechutama akikamilisha kazi yake ya shuleni bi Torrefranca aliiambia runinga ya ABS-CBN katika mahojiano.
''kwa hakika ilinipatia changamoto kubwa niendeleee kufanya bidii katika kila jambo linalonikabili''
Muda mchache baada ya bi Torrefranca kuchapisha picha hiyo kwenye Facebook maelfu ya watu waliichapisha pia wakisema kuwa ilikuwa imewavutia sana.
Sasa wahisani wamejitokeza kwa wingi kufadhili elimu yake.
Mamake kijana huyo Christina Espinosa anasema kuwa Cabrera anapenda shule na masomo yake licha ya shida chungu nzima wanazokabiliana nazo hususan umaskini.

0 comments:

Post a Comment