Wednesday, July 1, 2015

"MAREKANI NA CUBA KUFUNGUA BALOZI"

www.pewainformation.blogspot.com
Marekani na Cuba zinatarajiwa kutangaza kufunguliwa kwa afisi za ubalozi katika miji mikuu pande zote ikiwa ni hatua kubwa ya kurejesha uhusiano wa kidiplomasia kati ya nchi mbili.
 Uhusiano kati ya Marekani na Cuba ulivunjika miaka ya sitini na Marekani iliiwekea Cuba vikwazo vya silaha. Hata hivyo nchi hizo zilikubaliana kurejesha uhsuano mwishoni mwa mwaka 2014.
mwezi Aprili Rais Barack Obama wa Marekani na mwenzake wa Cuba Raul Castro walifanya mazungumzo ya ana kwa ana ikiwa ni mara ya kwanza kwa nusu karne.
Marekani ilivunja uhusiano wake na Cuba mwaka 1959 baada ya Fidel Castro na Kakake Raul Castro kuongoza mapinduzi ualiyomuondoa madarakani Rais aliyeungwa mkono na Marekani Fulgencio Batista.

0 comments:

Post a Comment