Mtandao wa Wikileaks umesema kuwa una ushahidi kwamba baadhi ya maafisa wakuu wa taifa la Brazil walipelelezwa mara kadhaa na idara ya ujasusi nchini Marekani NSA.
Habari hizo zinasema kuwa Idara hiyo hususan ilipeleleza uchumi wa taifa hilo.
Wikileaks ilichapisha orodha ya nambari 29 za simu za raia wa Brazil waliopo katika sekta za benki,fedha na uchumi.Kulingana na mtandao huo udukuzi huo ulianza mapema mwaka 2011 na huenda hata mapema zaidi.
Rais
Dilma Rousseff alikatiza ziara yake mjini Washington miaka miwili
iliopita baada ya aliyekuwa mchambuzi wa maswala ya ujasusi Edward
Snowden kufichua kwamba simu zake pamoja na barua pepe zilikuwa
zikichunguzwa.
Uchapishaji huo ulibaini kwamba upelelezi huo
haukumlenga rais Dilma Rousseff pekee bali pia katibu wake,pamoja na
afisa mkuu wa idara ya wafanyikazi aliyekuwa waziri wa fedha Antonio
Palocci.Afisi yake ya nyumbani na hata simu zake katika ndege yake zilichunguzwa kwa mujibu wa Wikileaks.
"Marekani iliichunguza Brazil"