Ushirikiano unaoongozwa na
Marekani, unasema kuwa umefanya mashambulio makubwa ya ndege dhidi ya
shina la wapiganaji wa Islamic State, katika mji wa Raqqa, wa Syria.
Msemaji
wa Marekani, alieleza kuwa ndege zilishambulia mara 16, maeneo ya IS,
kwenye moja kati ya operesheni kubwa kabisa ya ndege kufanywa nchini
Syria.Alisema lengo haswa ni kuzuwia IS kutumia mji wa Raqqa, kuwa ndio makao ya shughuli zao, za kutuma wapiganaji wao nchini Syria na Iraq.
Shirika la kutetea haki za kibinaadamu la Syria, limesema kuwa shambulio la ndege ya Marekani isiyokuwa na rubani, ilipiga shule mjini Raqqa, na kuuwa raia watano, pamoja na mtoto, na mpiganaji mmoja wa IS.
"Majeshi ya muungano yashambulia IS Syria"