Lupita Nyong'o wa Kenya ametoka mbali tangu
alipopata tuzo ya Oscar ya mchezaji filamu bora msaidizi wa filamu ya
mwaka 2013 iitwayo ''Twelve Years a Slave''.
Uso wake umetawala kwenye ukurasa mbalimbali wa mwanzo wa majarida ya urembo,
ambapo amepata sifa tele kwa kipaji chake na mitindo pia.
Sasa Jambo ambalo wengi hawakujua ni kwamba alianza kuwa mwanaharakati
tangu utotoni, na hapa alikuwa akiimba kupambana na mauaji haramu ya
tembo.
DAWA MPYA YA UKIMWI KUKOSOLEWA.
Kwa muda mrefu wahudumu wa afya ya masuala ya ngono wamesisitiza matumizi ya mipira ya kondomu kama mbinu bora zaidi dhidi ya maambukizi ya virusi vya ukimwi.
Lakini tabia moja hatari ya kutumia madawa ya kulevya na wapenzi wa jinsia moja inazidi kuibua wasiwasi.
kumekuwa na njia nyingi za kinga dhidi ya virusi vya ukimwi, lakini kuna dawa moja mpya - Pre-Exposure Prophylaxis (PrEP) - ambayo inaweza kutoa kinga dhidi ya maambukizi ya ukimwi iwapo itatumika kabla ya kushiriki ngono.
Utafiti unaofanywa na daktari Sheena McCormack kutoka chuo kikuu cha London, unasema kwamba unapomeza dawa hiyo, inazuia maambukizi ya ukimwi kwa kuzuia ongezeko la virusi, hii ni baada ya majaribio kufanyiwa kundi moja la wapenzi wa jinsia moja, ambao wamo katika hatari kubwa zaidi ya maambukizi
Shirika la afya duniani limetambua kwamba dawa hiyo ya tembe inaweza kupunguza maambukizi kwa kiwango kikubwa.
Baadhi ya wakosoaji wanasema kuwa dawa ya aina hii inahamasisha watu wengi kushiriki ngono bila kutumia mipira ya kondomu
Hata hivyo matumizi ya dawa hii haizuii maambukizi ya magonjwa ya zinaa kama vile kisonono na kaswende, je, kukubalika kwa matumizi ya dawa hii duniani kunamaanisha ongezeko la magonjwa ya zinaa??
"Lupita Nyong'o:ateuliwa balozi wa kulinda Tembo"