Tuesday, July 7, 2015

China kuzuia kuporomoka kwa soko la hisa

Serikali ya China imeidhinisha hatua kadhaa mwishoni mwa juma kulishinikiza soko ambalo limepoteza takriban asilimia 30 ya thamani yake katika wiki tatu zilizopita.

Wakati hayo yakijiri - uwezo wa serikali hiyo kukopa unazidi kuwa katika hatari.
Ili kujaribu kuliimarisha soko- Beijing ilitangaza marufuku ya kuuzwa hisa mpya na kuamuru fedha nyingi kununua hisa zaidi.Lakini wawekezaji wengi wana wasiwasi na suala kwamba takriban robo ya makampuni yalioorodheshwa yameomba kusitisha kuuza hiza zao.
Hili linaonekana kama hatua ya kuyalinda makampuni hayo dhidi ya hasara zaidi.
Katika mwaka uliopita serikali ilifurahia uwekezaji katika soko la hisa na kupata faida zaidi ya mara mbili.Ilionekana kwamba ni mageuzi makuu kiuchumi kuyaacha masoko kutoa fedha kwa makampuni hayo kuliko serikali kufanya hivyo.
Lakini sasa viongozi wa serikali wanajaribu kuzuia soko kuporomoka, jambo wanalohofia huenda likasababisha ghasia za kijamii miongoni mwa wawekezaji milioni tisiini nchini humo.

0 comments:

Post a Comment