Wanamgambo wa Al Shabaab wamesema kuwa ni wao waliotekeleza shambulizi
Kaskazini Mashariki mwa Kenya ambapo watu 14 waliuawa usiku wa kuamkia
jumanne.
Shambulio hilo linaaminika kuwalenga wafanyikazi wa machimbo ya mawe wasiokua wenyeji wa mkoa huo.Shirika la msalaba mwekundu linaongoza oparesheni ya kuwaokoa majeruhi ambao idadi kamili haijulikani .
Wanamgambo wa Al shabaab wamekuwa wakilenga wakaazi wasio wenyeji wa asili katika eneo hilo katika mashambulio yaliyotangulia.
Shambulio kama hilo dhidi ya wachimba migodi lilitokea jijini Mandera mwezi Disemba 2014, ambapo takriban watu 36 waliuawa na wengine wengi kujeruhiwa.Mashambulio kama haya yametishia kudumaza shughuli za maendeleo na kiuchumi katika eneo la Kaskazini Mashariki mwa Kenya ambapo wengi wa wafanyikazi wake ni watu kutoka maeneo mingine ya Kenya.

Al Shabaab yadai ndio walioua watu 14 Kenya