Mamia ya wakimbizi wa Eritrea wanaoishi nchini Ethiopia wameandamana
mbele ya majengo ya muungano wa afrika AU wakiitaka muungano huo
kuchukua hatua zaidi kumaliza ukiukaji wa haki za kibinadamu nchini
mwao.
Wakiwa wamebeba mabango ya kumkashifu rais wa nchi hiyo, Isaias
Afeworki, waandamanaji hao wamesema ukiukaji mkubwa wa haki zao
umeendelea nchini Eritrea huku jamii ya kimataifa ikijikokota kuingilia
kati.
Ripoti ya hivi karibuni ya Umoja wa Mataifa imesema nchi hiyo inatawaliwa kwa hofu na woga mwingi.
Kiongozi
wa uchunguzi wa umoja wa mataifa ameitaka mahakama ya makosa makuu ya
kivita ICC kuchunguza tuhuma dhidi ya utawala wa rais Afeworki.
No comments:
Post a Comment