Serikali ya Afrika Kusini imekana ripoti kwamba mawaziri wake walipanga
njama ya kumtorosha rais wa Sudan Omar El Bashir wiki iliopita.
Nusra rais huyo akamatwe kufuatia agizo la mahakama ya kimataifa
kuhusu uhalifu wa kivita dhidi yake kutokana na mashtaka ya mauaji ya
kimbari.
Mahakama ya Afrika Kusini ilimuagiza Bashir kusalia nchini humo huku ikijadiliana kuhusu iwapo agizo hilo litekelezwe.
Lakini kabla ya mahakama hiyo kutoa uamuzi wake bwana Bashir aliondoka nchini Afrika Kusini na kurudi nyumbani.
Rais
huyo wa Sudan alikuwa nchini Afrika Kusini kwa mkutano wa viongozi wa
bara Afrika na kwamba serikali ilikuwa inajua kwamba ilihitajika
kumkamata kwa kuwa mwanachama wa ICC.
No comments:
Post a Comment