Kitengo cha polisi wa Ulaya kinabuniwa ili kuwatambua watu wanaotumia
mitandao ya kijamii kuwaingiza vijana wa kiislamu kupigania Islamic
State.
Kitengo cha Ulaya cha polisi Europol kinasema kuwa kuna zaidi ya ujumbe
laki moja katika twitter unaotumwa kila siku katika kurasa zinazohusiana
na kundi hilo ambalo linathibiti Syria na Iraq.
Kitengo hicho kipya kitajaribu kufutilia mbali kurasa za IS kwa muda wa saa mbili pindi zinapotambuliwa.
Europol
inaamini kuwa zaidi ya raia elfu tano wa muungano wa ulaya kutoka nchi
za Uingereza, Ufaransa, Ubelgiji na Uholanzi wamezuru maeneo
yanayotawaliwa na Islamic State.
No comments:
Post a Comment