Wednesday, June 24, 2015

Kitengo cha ujasusi nchini Marekani NSA kiliwachunguza marais wa Ufaransa akiwemo Jacques Chirac,Nicolas Sarkozy na Francois Hollande mwaka 2006-12,kulingana na mtandao wa wikileaks
Mtandao huo ulipata habari hizo kutoka kwa ripoti za kiintelijensia na stakhabadhi nyengine za kiufundi za NSA.
Afisa mmoja wa Ufaransa amesema kuwa upelelezi wa washirika haufai.
Rais wa Ufaransa Francois Hollande anatarajiwa kujadili swala hilo na maafisa wa usalama.
Marekani haijathibitisha ukweli wa stakhabadhi hizo.

0 comments:

Post a Comment