Wakazi wa kitongoji duni cha Mathare
katika mji mkuu wa Kenya, Nairobi, sasa wanaweza kupata maji safi ya
kunywa na kwa matumizi mengine.
Mpango unaoungwa mkono na serikali
umezinduliwa kwenye mji mkuu wa Kenya Nairobi unaowawezesha watu
wanaoishi kwenye mitaa ya mabanda kununua maji kwa kutumia kadi.Vituo vya kuuza maji vimebuniwa kote katika sehemu za mabanda ambapo wenyeji hutumia kadi zilizo na pesa kununua maji safi na kwa bei nafuu.
HATIMAYE MAJI YA ATM YAZINDULIWA NCHINI KENYA!