Afrika Kusini imesema kuwa huenda ikajiondoa kutoka kwa mahakama ya
kimataifa ya uhalifu wa kivita ICC yenye makao yake makuu huko Hague
Uholanzi kufuatia jaribio la kumkamata rais wa Sudan Omar al Bashir
alipokuwa nchini humo majuzi.
Hata hivyo Nusra akamatwe kufuatia agizo la mahakama ya kimataifa
kuhusu uhalifu wa kivita dhidi yake kutokana na mashtaka ya mauaji ya
kimbari.Lakini baada ya kikao maalum cha baraza la mawaziri nchini humo, serikali ilitoa onyo kuwa huenda ikalazimika kujiondoa kutoka kwa makubaliano yeyote na mahakama ya ICC kutokana na sababu kadha.
AFRICA KUSINI HUENDA IKAJIONDOA KATIKA ICC