Wapiganaji wengi wa Kiislam wa kundi la Islamic State wameripotiwa
kuuawa katika mapigano makali kati ya majeshi ya usalama ya Misri na
kikundi hicho katika peninsula ya Sinai, kaskazini mwa Misri. Mapigano
yalidumu kwa saa kadha kuzunguka mji wa Sheikh Zuwaid, kwa serikali
kupeleka ndege na helikopta za kivita.
Mbali na kuuawa kwa wapiganaji wa Islamic State, wanajeshi na raia ni miongoni mwa waliopoteza maisha.
Habari
kutoka mjini Cairo, Majeshi maalum ya usalama ya Misri yalizingira
jengo moja na kuwaua wafuasi tisa wa kikundi cha Muslim Brotherhood.
Wizara ya mambo ya ndani imesema watu hao walishukiwa kupanga mfululizo
wa mashambulio. Kikundi cha Muslim Brotherhood kimesema wafuasi wake
tisa waliuawa kikatili na kimewataka wafuasi wake kufanya maasi dhidi ya
Rais Abdel-Fattah el-Sisi.
Wapiganaji wa Islamic State wamekuwa
pia wakiendesha mashambulizi katika nchi za Syria na Iraq kwa lengo la
kuzitawala nchi hizo.
No comments:
Post a Comment