Paka mmoja wa Japani ambaye alipata umaarufu alipofanywa kuwa mkuu wa
kituo cha reli, amefariki, na waombolezaji wengi wamejitokeza
Wakuu na washabiki walihudhuria mazishi ya paka huyo, katika kituo cha reli, ambako alitumika.
Paka
huyo aliyejulikana kwa jina ''Tama'' ambaye alipatikana akiranda randa
katika kituo cha reli cha Kishi miaka minane iliyopita kabla yake
kutawazwa kuwa meneja wa kituo hicho,
aliaga dunia majuzi kutokana na umri wake mkubwa wa miaka 16.
Tama
aliishi katika kituo hicho akiwa amevalia sare rasmi ya afisa mkuu wa
kituo cha reli na kuibuka kuwa kivutio kikubwa cha watalii.
Alivishwa kofia na kikoti maalumu alichoshonewa.
Viongozi
na wananchi wa matabaka mbalimbali walimmiminia sifa paka huyo hasa
wakisema kuwa ndiye aliyefufua kituo hicho cha reli.
Rais wa
shirika la reli ya umeme la Wakayama Japan , bwana Mitsunobu Kojima,
alimsifu Tama kwa kufufua uchumi katika eneo zima la Wakayama.
No comments:
Post a Comment