Ripoti kutoka Somalia zinasema kuwa kundi la wapiganaji wa jihad nchini
humo Al Ashabaab limevamia kambi moja ya kijeshi na kuwaua takriban
wanajeshi 10.
Walioshuhudia wanasema kuwa kulikuwa na mapigano makali karibu na kambi hiyo katika mji wa bandari wa Kismayu.
Alshabaab
limeimarisha mashambulizi yake dhidi ya wanajeshi wa Somalia na wale wa
Umoja wa Afrika wakati wa mwezi mtukufu wa Ramadhan.
Wakaazi wa
jimbo la kusini mwa Lower Shebelle wanasema kuwa vikosi vya Umoja wa
Afrika vimejiondoa katika kambi zake katika maeneo hayo.
Kufikia sasa hakuna tamko lolote kutoka kwa jeshi la umoja huo.
No comments:
Post a Comment