Shirikisho la soka nchini Tanzania (TFF) limepitisha azimio la kila
mchezaji wa kigeni kulipa dola 2,000 ( wastani wa milioni 5) kwa kila
msimu atakaocheza ligi kuu ya Tanzania.
Wachezaji wa kigeni waliosalia kuendelea kuchezea timu zao na wale
wanaosajiliwa kwa ajili ya msimu ujao watalazimika kulipa kiasi hicho
cha pesa.
Msemaji na afisa habari wa TFF, Baraka Kizuguto amesema
maamuzi ya kikao cha kamati ya utendaji ya TFF kilichoketi Jumamosi
visiwani Zanzibar ni kuwa kiasi hicho cha pesa kitakuwa ni kwa ajili ya
kuendeleza mpira wa miguu nchini Tanzania.
Katika miaka ya nyuma,
wachezaji wa kigeni kutoka nchi mbalimbali, hasa za Afrika ya Mashariki,
Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi walikuwa hawatozwi kiasi chochote cha
pesa licha ya kulipwa mamilioni.
Kizuguto amesema fedha hizo zitapelekwa katika mfuko wa maendeleo ya mpira wa miguu ujulikanao kama (Football Development Fund)
No comments:
Post a Comment