Wanamgambo wa kundi la Islamic State wametoa kanda ya video wanayosema
inaonyesha mauaji ya takriban Wakristo 30 kutoka Ethiopia waliokamatwa
na washirika wa IS nchini Libya.
Picha za kundi moja zimeonyesha wakikatwa vichwa katika ufukwe wa
bahari huku picha nyengine zikionyesha kundi jingine la raia hao
wakipigwa risasi kichwani katika jangwa.
Maandishi katika kanda hiyo yanasema kuwa waathiriwa ni wanachama wa kanisa la Ethiopia.
Kanda
hiyo ya dakika 29 inaonyesha alama ya kundi la mawasiliano la IS kwa
jina Al-Furqan na inafanana na ile iliotolewa hapo awali na kundi hilo
ikiwemo ile iliochapishwa mwezi Februari ambayo ilikuwa ikiwaonyesha
wapiganaji wa kundi hilo wakiwakata vichwa wakristo 21 wa Misri katika
ufukwe wa bahari nchini Libya.
No comments:
Post a Comment