Maofisa wa afya nchini Sierra Leone wamesema kwamba kuna wagonjwa wawili
wapya wanaougua ugonjwa wa ebola na kwamba wamegunduliwa katika mji
mkuu wa nchi hiyo Freetown.
Hapo awali ilidhaniwa kwamba mji huo ulikuwa hauna maambukizi ya
ugonjwa huo,na hakukuwa na wagonjwa walioripotiwa hapo kabla kwa muda wa
wiki kadhaa.
Naye msemaji wa kituo cha karantini cha taifa hilo
amesema kwamba kulikuwa na wasiwasi mkubwa kwasababu vituo vyote vya
karantini na vitendea kazi vyake vilikuwa vimefungwa mjini Freetown.
Na akaongeza kusema kwamba kuna shaka kuwa kutatokea maambukizi mapya kutoka katika eneo lenye msongamano wa makazi duni.
Nako upande wa Kaskazini mwa nchi hiyo ya Sierra Leone unaendelea kupata maambukizi mapya ya ugonjwa.
No comments:
Post a Comment